Tuesday, March 21, 2017

Apigwa ngumi akidaiwa kuuza stika feki za bima

By Burhani Yakub, Mwananchi

Tanga. Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakala mmoja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) jijini hapa, amepigwa ngumi na mteja wake akidaiwa kuuza stika bandia ya bima.

Walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa mteja huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, alikasirishwa na kitendo cha kutoonyeshwa stika kama ni halali alipofanya uhakiki mtandaoni.

Hata hivyo, Kaimu Meneja wa NIC Tawi la Tanga, Abdul Kufakunoga alisema aliyepigwa ni wakala wa shirika hilo na stika alizotoa ni halali.

Katibu Muhtasi wa wakala huyo, Hadija Chonge alisema licha ya kumuelewesha mteja kuwa  stika aliyopewa ni halali iliyotolewa na NIC, lakini hakutaka kuelewa.

-->