Ushauri damu ya wanyama itumike kwa binaadamu

Muktasari:

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa ulifanyika wilayani Arumeru chini ya mkuu wa mkoa wa huo, Mrisho Gambo alisema kutokana na changamoto kubwa inayoikabili Wizara ya Afya katika kuijihakikishia usalama wa damu ni bora uangaliwe utaratibu wa kutumia damu za wanyama.

Arusha. Katibu Tawala Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Robert Siyantemi ameshauri tafiti za kisayansi zifanyike ili kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kwa binadamu.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa ulifanyika wilayani Arumeru chini ya mkuu wa mkoa wa huo, Mrisho Gambo alisema kutokana na changamoto kubwa inayoikabili Wizara ya Afya katika kuijihakikishia usalama wa damu ni bora uangaliwe utaratibu wa kutumia damu za wanyama.

"Mheshimiwa mwenyekiti naamini utafiti umeshafanyika au unaendelea kufanyika nashauri damu za wanyama hasa hawa wanaofanania na binadamu kama nyani, tumbili na kima damu zao zifanyiwe utafiti tuone kama zinaweza kutusaidia," alisema

Siyantemi ambaye alikua miongoni mwa wanachama 42 wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)waliomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea urais mwaka 2015 alijizolea umaarufu akiwa mtia nia kijana kuliko wote.