Asilimia 69 ya Watanzania wanakabiliwa na njaa

Muktasari:

Matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza Februari yanaonyesha kuwa asilimia 51 ya kaya hazikuwa na Chakula chankutosha au mwanakaya ameshinda njaa kwa sababu hakuweza kupata Chakula.

Dar es Salaam. Asilimia 69 ya Watanzania wanakabiliwa na uhaba wa chakula tangu mwakan2016, utafiti umeeleza.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza Februari yanaonyesha kuwa asilimia 51 ya kaya hazikuwa na Chakula chankutosha au mwanakaya ameshinda njaa kwa sababu hakuweza kupata Chakula.

Akifafanua kuhusu utafiti huo leo Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema takwimu zake zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania Bars kati ya Septemba 14-26, 2016 nabkutoka kwa wahojiwa 1,610 kati ya February 9-15, 2017.

"Kwa mujibu wa wananchi wengi, Uhakika wa kupata chakula umepungua kati ya Septemba 2016 na February 2017. Asilimia 65 ya wananchi walikuwa na hofu ya Maya zaobkukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na asilimia 45 waliosema hiyo Septemba 2016," alisema Eyakuze.

"February 2017 asilimia 51 ya wananchi waliripoti kwamba kuna wakati hawakuwa na Chakula ch kutosha  kwa ajili ya kaya zao katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita," aliongeza.