Askari wanaoendekeza dawa za kulevya kukiona

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba 

Muktasari:

Akizungumza na maofisa wa polisi na magereza wilayani Tarime mkoani Mara, Nchemba amesema hafurahishwi na vitendo vya askari wanaotajwa kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Tarime. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hatawafumbia macho askari wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na tayari dawa dhidi yao imepatikana.

Akizungumza na maofisa wa polisi na magereza wilayani Tarime mkoani Mara, Nchemba amesema hafurahishwi na vitendo vya askari wanaotajwa kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Nchemba amelitaka jeshi hilo kufuata maadili ya kazi na kulinda heshima yao, raia na mali zao.

 “Wanaofanya vitendo hivi wanafahamika maana wapo ndani ya jamii, tufanye kazi kwa ustadi mkubwa ili tuwabaini na kuwafikisha kwenye sheria wasifanye uhalifu huu,” amesema Waziri.