Askofu Nyaisonga rais mpya wa TEC

Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Gervas Nyaisonga

Muktasari:

  • Ametangazwa leo mjini Sumbawanga

Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) leo Jumapili Juni 24, 2018 limemchagua Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Gervas Nyaisonga kuwa rais wa baraza hilo.

Askofu Nyaisonga aliyetangazwa leo katika misa  ya kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, Beatus Urassa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania mjini humo, amechukua nafasi ya Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa aliyemaliza muda wake.

Ngalalekumtwa amemtangaza Askofu Nyaisonga na kusema atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.