Aumwa na buibui mara mbili kwenye uume

Muktasari:

Kijana huyo mwenye miaka 21jana aling’atwa kwa mara ya pili alipokuwa anajisaidia  katika eneo ambalo ujenzi unaendelea . uume wake uling’atwa pale pale alipong’atwa miezi mitano iliyopita.

Huenda akawa na mkosi au  waswahili wangesema amerogwa. Mwanaume  mmoja nchini Australia, ameumwa na mdudu aina ya buibui  mwenye sumu kali mara  mbili  kwenye uume wake.

Kijana huyo mwenye miaka 21jana aling’atwa kwa mara ya pili alipokuwa anajisaidia  katika eneo ambalo ujenzi unaendelea . uume wake uling’atwa pale pale alipong’atwa miezi mitano iliyopita.

Jordan, alikaririwa na mtandao wa gazeti la Metro la Uingereza lakini hakutaka kutaja jina lake la ili na kusema aliumwa pale pale alipoumwa mara ya kwanza.

 Aliumwa na bui bui huyo mkali mwenye sumu aina ya ‘redback’ ambaye anaweza kuua iwapo hautapata tiba ya kuondoa sumu.

"Nilikuwa nimeketi chooni nikiendelea na shughuli zangu nilipohisi uchungu wa ghafla kama niliouhisi wakati ule. Sikuamini kwamba limefanyika tena. Niliangalia chini na nikaona miguu kadha imechomoza."

Amesema tangu alipoumwa mara ya kwanza, amekuwa akihofia sana kutumia vyoo vya muda.

"Baada ya kisa hicho cha kwanza, kusema kweli sikutaka kuvitumia tena," anasema.

"Vyoo huoshwa siku hiyo na nilifikiria ilikuwa wakati mwafaka kwangu kuvitumia. Niliangalia vyema chini kabla ya kuketi kuanza shughuli yangu. Kushtukia, mimi huyo naumwa tena."

Mwenzake alimkimbiza hospitali ya Blacktown.

Alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani lakini kuna uwezekano kwamba huenda asitumie vyoo vya muda tena.

Mtu anapoumwa na buibui hupata maumivu makali, kutokwa na jasho na pia kupata kichefuchefu.

Ingawa kumewahi kuripotiwa visa vya watu kufariki baada ya kuumwa na buibui aina ya redback, hakuna aliyefariki tangu kugunduliwa kwa dawa ya kumaliza sumu mwaka 1956.