Azam Marine, Kilimanjaro zasitisha safari za boti Dar- Zanzibar

Kaptani wa Boti za Kampuni ya Azam Marine, Feruzi Kassim anayehusika  na kuhakikisha Boti zinaendeshwa kwa usalama na kulinda uchafuzi ya Bahari akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusianaa na kusitisha kwa safari za Boti kwenda Zanzibar kutokana na hali ya hewa. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries zimesitisha safari za boti kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar kutokana na hali ya upepo baharini.


Dar es Salaam. Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries zimesitisha safari za boti zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar kutokana na hali ya upepo baharini.

Kampuni hizo zimefikia uamuzi huo baada ya Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Hali ya Hewa (Zanzibar) kutoa taarifa zikieleza kuwa hali ya hewa si salama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo safari hizo zimesitishwa leo Jumanne Oktoba 23, 2018.

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi