Azam Media waachana na Lulu

Muktasari:

Lulu kwa sasa anatumiki akifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia Steven Kanumba. Muigizaji huyo alihukumiwa mwaka jana.


Kampuni ya Azam Media imetangaza kusitisha mkataba na muigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael “Lulu” wa kuwa balozi wa tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) kutokana na matatizo yaliyomkuta.

Lulu kwa sasa anatumiki akifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia Steven Kanumba. Muigizaji huyo alihukumiwa mwaka jana.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema hakutokuwa na balozi mwingine kwa sababu mchakato wake unachukua muda mrefu.

Mhando amesema kuwa walishindwa kuweka wazi suala hilo kutokana na mambo mbalimbali na wakati umefika kwani watu wengi walikuwa wanahoji hatma ya mkataba wa kampuni yao na Lulu.

“Huo ni uamuzi wa kampuni na ulifikiwa baada ya kuhukumiwa, kwa hiyo nafasi ya ubalozi wa tuzo za SZIFF haipo,” amesema Mhando.