Azam wataka mechi za Simba, Yanga Chamazi

Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd 

Muktasari:

Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd amesema  wameandika barua kwa TFF wakitaka michezo yao ya nyumbani dhidi ya timu hizo ifanyike Chamazi na si Uwanja wa Taifa kama ilivyozoeleka.

Dar es Salaam. Uongozi wa Azam  umeliandikia barua Shirikisho la Soka  Tanzania (TFF) kuomba michezo yake ya  nyumbani ya Ligi Kuu dhidi ya Simba na Yanga ifanyike kwenye Uwanja wa Azam  Complex, Chamazi.

Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd amesema  wameandika barua kwa TFF wakitaka michezo yao ya nyumbani dhidi ya timu hizo ifanyike Chamazi na si Uwanja wa Taifa kama ilivyozoeleka.

 “Uwanja wa wetu umekidhi vigezo vyote vinavyostahili kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Shirikisho la Soka Afrika (CAF),” amesema Idd.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas hakuwa tayari kuthibitisha taarifa hizo.