LIVE: Familia ya Mo Dewji inazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Muktasari:

  • Leo mchana familia ya Mo Dewji na kampuni anazoziongoza itazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam.

Dar es Salaam. Familia ya mfanyabiashara maarufu , Mohammed Dewji ‘Mo’ na Kampuni Tanzu za Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) leo Jumatatu Oktoba 15, 2018 watazungumza na waandishi wa habari kuhusu kutekwa kwa bilionea huyo.

Mkutano huo na waandishi unatarajia kufanyika saa 6.30 mchana katika ofisi za MeTL zilizopo jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es Salaam.

Baba wa ‘Mo’ Gullam Dewji amethibitisha uwepo wa mkutano huo na waandishi wa habari wa vyombo vya ndani na nje ya nchi.

Soma zaidi

Gullam ameliambia Mwananchi leo asubuhi kuwa watazungumzia tukio la kutekwa na kupotea kwa mwanae.

Mkutano huo unafanyika ikiwa ni siku ya tano leo tangu kutekwa na watu wasiojulikana kwa Mo Dewji, Alfajiri ya Alhamisi Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Collosseum jijini Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi