Sirro aapishwa kuwa IGP mpya

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemuapisha mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua nafasi ya Ernest Mangu.

Hafla hiyo imeudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba na makamishna mbalimbali wa jeshi hilo.

Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.