Baraza la wadhamini lamtaka Makonda kusimamisha mkutano wa dharura Simba

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Muktasari:

Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Hamis Kilomoni amesema baraza hilo limefikia hatua hiyo baada ya kupokea barua za  malalamiko kutoka kwa wanachama.

Dar es Salaam. Baraza la wadhamini la klabu ya Simba limemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuingilia kati na kuusimamisha mkutano mkuu wa dharura mpaka uongozi utakapokutana na baraza hilo.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Hamis Kilomoni amesema baraza hilo limefikia hatua hiyo baada ya kupokea barua za  malalamiko kutoka kwa wanachama.

"Kama wadhamini tumepokea barua za wanachama wakilalamikia kutoitwa katika mkutano uliopita. Barua hizo zimepelekwa kwa rais,BMT hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa aingilie katika na kusimamisha mkutabo mpaka viongozi wakutane nasi,"amesema

Kilomoni amesema baraza la wadhamini halitambua mkutano huo na kwamba ni batili.