Basata laufungia wimbo wa Nay Mitego

Muktasari:

Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Mngereza amesema hayo leo (jumatatu) na kueleza kuwa wimbo ulioimbwa na msanii huyo usitumike kwa namna yoyote ile kwa kuwa umevunja sheria ya Sanaa. 

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeufungia rasmi wimbo "Wapo" wa msanii Elibariki Emmanuel maarufu kama Nay wa Mitego. 

Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Mngereza amesema hayo leo (jumatatu) na kueleza kuwa wimbo ulioimbwa na msanii huyo usitumike kwa namna yoyote ile kwa kuwa umevunja sheria ya Sanaa. 

"Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L)cha sheria ya Basata namba 23 ya mwaka 1984,baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali zisizo salama, "alisema Mngereza. 

Aidha Baraza limewaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi.