Bashiru Ali asema wanaosubiri kumzomea, kumpima, si wana CCM

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally . Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Amezungumzia mabadiliko ndani ya CCM na kusema ataanzia pale Kinana alipoishia.


Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema wale wanaosubiri kumzomea na kupima uwiano wake na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana hao ni mashabiki na si wana CCM.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Juni 19, 2018 katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga Kinana na kumkaribisha yeye (Bashiru) iliyofanyika jijini Dodoma.

“Kuondoka kwa Kinana kumeleta wasiwasi tusidanganyane,  na sasa mnayasubiri matarajio kutoka kwa Bashiru, lakini si  Kinana wala Bashiru tunaoweza kuleta uwiano sawa lakini kama kuna watu wamekaa tayari kumzomea Bashiru kusubiri kuona uwiano wa Kinana na Bashiru hao si wana CCM, ni mashabiki,” amesema Dk Bashiru.

Katika kusisitiza hilo, amesema, wana CCM hawana budi kufikia kule  chama kinapokwenda.

“Nawaahidi nitaanzia pale alipoishia Kinana  kuongoza mapambano ya chama chetu ili wale wanaosubiri kuona tukiyumba washindwe.”amesema

Amezungumzia mabadiliko ndani ya CCM na kusema ataanzia pale Kinana alipoishia.

 “Nimekuja tuzungumze, ili tuanze kazi pale alipoishia Kinana. Katika chama kikubwa  kama CCM, kna mabadiliko makubwa mawili, wasiwasi na matarajio,”amesema

Amesema mabadililiko husababisha msisimiko wa matarajio makubwa na upande mwingine, mabadiliko huwa na tabia ya kuzaa

Katika hafla hiyo, Kinana na Bashiru kwa pamoja wamezawadiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa wabunge. Baadhi ya zawadi hizo ni ng’ombe, mbuzi, kahawa, mafuta ya kula, korosho huku Kinana akipewa gari aina ya Voxy na wabunge hao.