Basi, lori yateketea Dar

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda

Muktasari:

Ajali hiyo ilihusisha basi la Safari Njema lililokuwa linatokea Dodoma  na lori lililokuwa limebeba saruji.

Dar  es Salaam. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea jana eneo la kati ya Stop Over na- Kimara Suka, jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilihusisha basi la Safari Njema lililokuwa linatokea Dodoma  na lori lililokuwa limebeba saruji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda alisema mtu mmoja ambaye  hajatambuliwa alifariki dunia, lakini majeruhi 10 walipelekwa Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH).

“Tunafuatilia chanzo cha ajali hiyo, lakini magari yote mawili yameteketea kabisa kwa moto. Abiria wengi wamepona katika ajali hiyo,” alisema kamanda huyo akiwa  eneo la tukio.