Basi la New Force laanguka Mlima Kitonga

Muktasari:

Basi la kampuni ya New Force leo mchana Oktoba 16, 2018 limetumbukia katika Mlima Kitonga mkoani Iringa


Dar es Salaam. Basi la kampuni ya New Force lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam limeanguka  katika mteremko wa Mlima Kitonga mkoani Iringa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali imetokea na RTO (mkuu wa usalama barabarani wa mkoa) anakwenda eneo la tukio. Lakini taarifa za awali kuna majeruhi tu.”

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi