bei ya korosho yaendelea kuongezeka

Muktasari:

Katika mnada wa kwanza uliofanyika leo katika ukumbi wa halmshauri ya Tandahimba korosho zilizouzwa ni  tani 6,225.

Tandahimba. Bei ya zao la korosho katika chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba-Newala Corporative Union (Tanecu) imepanda kutoka Sh 3,650 ya msimu wa mwaka 2016/17 na kufikia Sh 3,850 hadi Sh 3,800 kwa msimu mpya wa mwaka 2017/18.
Katika ghala la Newala tani 2,800 zimeuzwa kwa bei ya Sh 3,850 hadi Sh 3,800 huku ghala la Tandahimba zilizouzwa ni tani 3,425 kwa bei ya Sh 3,810 hadi Sh 3,800 baada ya baadhi ya wakulima walioshiriki katika mnada kuridhia bei hiyo baada ya kupitia bahasha 54 za tender box.
Msimu wa ununuzi wa korosho ghafi za wakulima kitaifa ulifunguliwa rasmi Oktoba Mosi mwaka huu. Mkutano huo ulitangaza bei dira kwamba Sh 1,450 kwa korosho daraja la kwanza (Standard grade) na Sh 1,160 kwa korosho daraja la pili (Under grade)
Kwa mujibu wa bodi ya korosho hadi kufikia Oktoba 16 jumla ya wanunuzi 76 walijitokeza na kupatiwa leseni ambapo 47 walisajiliwa na kupatiwa leseni za ununuzi.
Pia, katika misimu iliyopita mwaka 2016/17 jumla ya korosho ghafi tani 264,887.527,msimu wa 2015/16 tani 155,244.645, mwaka 2014/15 tani 197,932.501,mwaka 2013/14 tani 130,123.778 na mwaka 2012/13 tani 127,947.473
Aidha mkoa wa Mtwara umekusanya na kuuza korosho ghafi zipatazo tani 172,771.109, kwa mwaka 2016/17,2015/16 tani 106,940.222, mwaka 2014/15 tani 131,781.799,mwaka 2013/14 tani 86,070.288 na tani 87,285.730 kwa mwaka 2012/13
Mkoa wa Lindi mwaka 2016/17 ulikusanya na kuuza tani 61,739.316,msimu wa mwaka 2015/16 tani 27,936.734, mwaka 2014/15 tani 46,101.346,msimu wa 2013/14 26,647.980 na msimu wa 2012/13 tani 34,968.240.
Ruvuma msimu wa mwaka 2016/17 tani 15,429.183,msimu wa mwaka 2015/16 tani 10,528.716, mwaka 2014/15 tani 8,262.229,mwaka 2013/14 tani 11,572.793 na mwaka 2012/13 tani 3,178.340.
Mkoa wa Pwani msimu wa mwaka 2016/17 tani 13,265.861,mwaka 2015/16 tani 8,081.727, na msimu wa mwaka 2014/15 tani 9,627.314.
Mikoa mingine ni Tanga msimu wa mwaka 2016/17 zilizokisanywa na kuuzwa ni tani 682.058 na msimu wa mwaka 2015/16 ni tani 344.
Katika mkoa wa Mbeya jumla ya tani 138.352  zilikusanywa katika msimu wa mwaka 2016/17 na tani 344 kwa msimu wa mwaka 2015/16 huku mkoa wa Njombe ukikusanya na kuuza tani  80.429 kwa msimu wa 2016/17 na tani 5.00 kwa mwaka 2015/16
Mikoa mingine iliyokusanya na kuuza korosho ghafi kwa msimu 2016/17 ni Iringa tani 451.360,Morogoro tani 102.590,Dodoma tani 19.521 na Singida tani 207.748.