Wednesday, March 15, 2017

Benki ya UBA yazindua ATM nne

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Benki ya UBA tawi la Tanzania leo (Jumatano) imezindua mashine nne za kutolea fedha katika maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kujiongezea wigo wa kuwafikia wateja wao.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine huo uliofanyika jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma amesema wameamua kujitanua ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wateja wao.

“Ni wajibu wetu kuwasogezea huduma wateja wetu, kabla ya hapo mashine za ATM zilikuwa katika matawi yetu matatu yaliyopo jijini hapa, “ amesema Jenerali Mboma.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Peter Makau amesema wanalenga kupanua wigo na kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa.

“Kuwasogezea huduma hii kutawasadia wananchi kuwa karibu na fedha zao na ule muda waliokuwa wakiutumia kuziafuata umbali mrefu, watautumia katika shughuli nyingine za maendeleo,” amesema Makau.

Benki hiyo imezindua mashine za kutolea fedha katika maeneo ya Mabibo (Oil Com), Tabata Segerea (Oil Com), Mbezi Beach (Oil Com) na Mkuki Mall.

-->