Biashara ya magari kaa la moto

Magari yakiwa yamewekwa katika yadi kwa ajili ya kuuzwa. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla iliyoandaliwa na CCM mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi mwaka 2010.

Dar es Salaam. Wakati fulani, Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete aliwahi kusema ongezeko la foleni za magari jijini Dar es Salaam ni uthibitisho tosha wa maisha bora.

Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla iliyoandaliwa na CCM mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi mwaka 2010.

Wakati huo biashara ya magari ilikuwa imeshamiri na wafanyabiashara wa eneo hilo walikuwa wakitengeneza fedha nyingi huku yadi za kuuzia magari, mengi yakiwa ni mitumba, zikiongezeka kila kona ya jiji la Dar es Salaam.

Lakini, hali imebadilika katika kipindi cha muda usiozidi miaka miwili; wauzaji wa magari sasa wanalalamikia biashara kudoda na wengine wanafikiria hata kufunga biashara hizo kutokana na kukauka kwa wateja.