BoT: Pato la taifa laongezeka kwa asilimia 6.7

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT)Benno Ndulu

Muktasari:

Nusu ya kwanza ya mwaka 2015 pato la taifa liliongezeka kwa asilimia 5.7.

Dar es Salaam.  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT)Benno Ndulu amesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 6.76 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari hadi Juni)  ukilinganisha na kipindi hicho mwaka jana.

Nusu ya kwanza ya mwaka 2015 pato la taifa liliongezeka kwa asilimia 5.7.

Sekta zilizoongoza kwa kukuza pato hilo ni Uchukuzi na uhifadhi mizigo iliyochangia asilimia 17.4, uchimbaji madini na gesi asilimia 13.7 sekta ya mawasiliano asilimia 13 na sekta ya fedha na bima kwa asilimia 13.

Makusanyo ya ndani yameongezeka kwa asilimia 34.