Bobali awapa darasa wafanyabiashara

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali

Muktasari:

  • Bobali alitoa ushauri huo kwenye mkutano na wafanyabiashara uliowashirikisha pia maofisa kutoka benki ya NMB na Jeshi la Polisi mkoani Lindi juzi.

Lindi. Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali amewashauri wafanyabiashara wa Kata ya Milola kutumia benki kuweka fedha ili kuepuka usumbufu wanapotaka mikopo.

Bobali alitoa ushauri huo kwenye mkutano na wafanyabiashara uliowashirikisha pia maofisa kutoka benki ya NMB na Jeshi la Polisi mkoani Lindi juzi.

Alisema wafanyabiashara wanapaswa kutumia rasilimali na biashara zao kujipatia mikopo katika benki hiyo kwa sababu ipo kwa ajili yao na wawe waaminifu.

“Nimelizamika kukutana nanyi ili kusikiliza kero zenu kuhusu mikopo na usalama wa biashara zenu ili kujua namna ya kuzitatua,” alisema Bobali.

Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo, Hadija Abdallah alimuomba mbunge huyo kushughulikia tatizo la ushuru wanaotozwa kwenye nazi jambo linalowarudishwa nyuma kiuchumi.

Kaimu Meneja Mikopo wa NMB Lindi, Robert Pazi alisema benki hiyo ipo tayari kutoa mikopo kwa atakayekidhi vigezo.

Mwakilishi wa Polisi Mkoa wa Lindi, Peter Msafiri aliwaahidi wafanyabiashara na wananchi kushirikiana nao kuhakikisha kituo kinajengwa na kukamilika kwa wakati.