Waziri aagiza bosi Bodi ya Korosho aondolewe kazini

Muktasari:

  • Wizara kutangaza wa kujaza nafasi hiyo.

Dodoma. Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, Mathew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa kaimu mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hassan Jarufu.

Waziri Tizeba alitoa agizo hilo jana Jumamosi Aprili 21, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk Tizeba ametangaza hatua hiyo, saa chache baada ya shughuli za uwekwaji jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Uwekaji jiwe la msingi ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 

“Tumechukua uamuzi huu baada ya kuangalia mwenendo wa Jarufu na kutafakari jinsi zao la korosho linavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuatilifu kwa wakati,” amesema

Dk Tizeba alisema wizara ya kilimo itamtangaza kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo kujaza nafasi hiyo.

Mwisho.