CCM, Chadema ng’adung’adu

Muktasari:

  • Katika matokeo ya awali ya uchaguzi huo, yanaonyesha mchuano mkali kati ya wagombea wa vyama hivyo, huku Chadema kikionekana kuongeza kwenye vituo takriban vyote.
  • Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa waandishi wetu, Chadema kinaoongoza vituo vya Doma Stoo, Mtake, Ngwambe, Shule Doma, Doma Kilosa, Doma Stendi.

Mvomero. Ng’adung’adu ni neno la vijana wa mitaani wanalotumia kuonyesha mpambano mkali kati wanaopambana, hali hiyo imejidhihirisha katika Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji Doma, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro uliofanyika leo kati ya CCM na Chadema.

Katika matokeo ya awali ya uchaguzi huo, yanaonyesha mchuano mkali kati ya wagombea wa vyama hivyo, huku Chadema kikionekana kuongeza kwenye vituo takriban vyote.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa waandishi wetu, Chadema kinaoongoza vituo vya Doma Stoo, Mtake, Ngwambe, Shule Doma, Doma Kilosa, Doma Stendi.

Kiti hicho kilikuwa kinashikiliwa na CCM na uchaguzi huo umefanyika kufuatia kufariki dunia mwenyekiti wake