CCM Z’bar kubadili mbinu

Muktasari:

Mabodi alisema hayo jana katika ziara yake ya kwanza tangu akabidhiwe madaraka aliyoifanya Mkoa wa Kusini Unguja. Alisema chama hicho kina nyenzo za kila aina zitakazotumika katika uwanja wa kisiasa.

Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdallah Juma Abdallah maarufu Mabodi amesema chama hicho kimejipanga kufanya siasa za kisayansi zenye ushindani wa sera, kitaaluma na ubunifu zitakazojenga mazingira ya ushindi mwaka 2020.
Mabodi alisema hayo jana katika ziara yake ya kwanza tangu akabidhiwe madaraka aliyoifanya Mkoa wa Kusini Unguja. Alisema chama hicho kina nyenzo za kila aina zitakazotumika katika uwanja wa kisiasa.
Alisema ili kufikia malengo hayo kila mwanachama, mfuasi wa CCM na wananchi   wanapaswa kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano.
Akizungumza na wanachama wa Tawi la CCM Mtende, aliwataka wafuasi wa chama hicho kufungua ukurasa mpya wa kuanzisha miradi ya maendeleo katika matawi yao ili kujitegemea badala ya kuwa tegemezi kwa wabunge, wawakilishi na madiwani.