CCM na chama cha Kikomunisti China kuimarisha ushirikiano

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo

Muktasari:

  • Ujumbe huo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC, Guo Jin Long utafanya mazungumzo rasmi na viongozi wa CCM.

 

  • Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo amesema kesho kiongozi wa ujumbe huo anakutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli, na baadaye kuelekea zanzibar kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein.

Dar es Salaam. Ujumbe wa watu 19 kutoka chama cha kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchi kwa ziara rasmi ya siku tatu inayolenga kuimarisha ushirikiano na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ujumbe huo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC, Guo Jin Long utafanya mazungumzo rasmi na viongozi wa CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo amesema kesho kiongozi wa ujumbe huo anakutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli, na baadaye kuelekea zanzibar kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein.

"Ziara hii ni mwendelezo wa ushirikiano kati ya vyama hivi viwili ambao umekuwepo tangu tulipopata uhuru. Tutafanya mazungumzo ya pamoja kubadilishana uzoefu," amesema Mpogolo.