CCM yajiandaa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhamia Dodoma

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa

Muktasari:

Amesema hayo leo wakati alipokutana na wajumbe wa halmashauri ya mkoa ya chama hicho.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amesema chama hicho kitasimamia na kushiriki kukamilisha maelekezo yote ya Serikali kuhamia Dodoma.
Amesema hayo leo wakati alipokutana na wajumbe wa halmashauri ya mkoa ya chama hicho.
"Halmashauri kuu ya mkoa tumeazimia kuifanyia kazi hotuba ya Rais John Magufuli pamoja na maelekezo yote katika mkutano mkuu," amesema.
Hata hivyo amesema CCM mkoa inaielekeza Serikali kutunga sheria inayoitambua Dodoma kuwa ni makao makuu ya nchi.
Amesema pia Serikali ihakikishe kuwa  inasimamia azma ya kuhakikisha majengo yote ya wizara za Serikali inajengwa Dodoma badala ya Dar es Salaam na kuongeza kasi ya upimaji wa viwanja.