CCM yampitisha aliyeachia ubunge Liwale kugombea tena

Muktasari:

Mgombea huyo alitangaza kujiuzulu ubunge kupitia CUF Agosti 13 na kutangaza kujiunga na CCM

Dar es Salaam. Zuberi Kuchauka amepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea ubunge Liwake katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 12.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humprey Polepole imesema Kuchauka amepitishwa leo na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana jijini Dodoma chini ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho  Zanzibar, Rais Dk Ali Mohamed Shein.

“Kikao cha Kamati Kuu Maalum pamoja na mambo mengine kimemteua Zuberi Mohamed Kuchauka kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Liwale,” amesema Polepole.

Amesema pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imeiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kushughulika na utatuzi wa shida za watu sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Kikao pia kimewapongeza wanachama wa CCM na wananchi hasa katika maeneo yenye uchaguzi mdogo kwa utulivu, mshikamano na kushiriki  kutumia haki yao ya kisiasa kuchagua viongozi wao katika ngazi ya majimbo