CCM yashinda kijiji, Chadema yashinda kitongoji Ifakara

Muktasari:

Uchaguzi huo ambao ulifanyika Ifakara na kumalizeka usiku wa kuamkia leo msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kijiji cha Kikwawila, Gaston Kavuta alimtangaza mgombea wa CCM, Shabani Salahange alipata kura 557 na kumshinda mpinzani wake wa Chadema, Odric Matimbwa aliyepata kura 528 huku mgombea wa NCCR-Mageuzi, Bakari Mkungundile akipata kura 2.

Ifakara. Chama cha Mapinduzi(CCM) kimefanikiwa kushinda uchaguzi wa uenyekiti wa Kijiji cha Kikwawila huku Chadema nayo ikifanikiwa kushinda uchaguzi wa Kitongoji cha Mbasa Mlimani.

Uchaguzi huo ambao ulifanyika Ifakara na kumalizeka usiku wa kuamkia leo msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kijiji cha Kikwawila, Gaston Kavuta alimtangaza mgombea wa CCM, Shabani Salahange alipata kura 557 na kumshinda mpinzani wake wa Chadema, Odric Matimbwa aliyepata kura 528 huku mgombea wa NCCR-Mageuzi, Bakari Mkungundile akipata kura 2.

Wakati huo huo msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kitongoji cha Mbasa Mlimani, Asmina Lewisi alimtangaza mgombea wa Chadema, Majuto Mnasi alishinda kwa kupata kura 346 na kumshinda mgombea wa CCM, Mohamed Ishikala aliyepata kura 321 na mgombea wa NCCR-Mageuzi akipata kura 4.