Friday, April 21, 2017

CUF chadai kubaini mbinu chafu dhidi yake

Mwenyekiti wa chama hicho, anayetambuliwa na

Mwenyekiti wa chama hicho, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba 

By Bakari Kiango,Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Wananchi  (Cuf), kimewaonya vijana waliopangwa kuvamia ofisi ya makao makuu ya chama Buguruni kutothubutu kufanya hivyo.

Onyo hilo limetolewa leo (Ijumaa) na  Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano wa chama hicho, Abdul Kambaya upande unaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kambaya aliyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi ya makao makuu cha Cuf, Buguruni.

Amesema utafiti walioufanya wamebaini kuwa asilimia kubwa ya kundi la vijana hao wametoka katika mkoa wa Arusha na wamekuja Dar es Salaam kwa ajili kutekeleza mpango wa wakishirikiana chama kimoja cha upinzani.

"Wasithubutu kukanyaga hapa ofisini tupo vizuri na tumejipanga kisawasawa.Hata hivyo tumeshatoa taarifa polisi ili wajue kinachoendelea dhidi ya vijana hao wenye nia ovu na chama hiki," amesema Kambaya.

-->