CUF yatumia Sh500 milioni kumjadili Profesa Lipumba

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui

Muktasari:

Mkutano huo ambao ulijadili ajenda moja tu ya kupitisha barua ya kujiuzulu Profesa Lipumba ulitumia takribani Sh 500 milioni kwa maandalizi

Dar es Salaam. Wakati vikao vya viongozi wa CUF vikiendelea kujadili kilichojitokeza katika mkutano wake mkuu maalumu, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui amesema wajumbe walikubali kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na kubadilika badilika kwake.

Mkutano huo ambao ulijadili ajenda moja tu ya kupitisha barua ya kujiuzulu Profesa Lipumba ulitumia takribani Sh 500 milioni kwa maandalizi

Jumapili iliyopita, mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea taarifa ya kujiuzulu Profesa Lipumba na kufanya uchaguzi kujaza nafasi yake na nyingine zilizokuwa wazi, ulivunjika baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na wanachama waliotaka barua ya kujiuzulu ya kiongozi huyo ibatilishwe kama alivyoomba na aendelee kuongoza chama hicho.

 

Habari zaidi soma

Gazeti la Mwananchi