CWT yaeleza sababu ya wanafunzi kufeli mtihani wa Taifa

Muktasari:

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, George Nyangusu alisema baadhi ya walimu wamekata tamaa, hivyo hufundisha ili kutimiza wajibu bila kujali iwapo wanafunzi wanaelewa wanachofundishwa.

Kahama. Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Shinyanga kimesema malimbikizo ya malipo ya madai ya walimu, zikiwamo fedha za uhamisho na nyongeza ya mishahara ni chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya kwenye mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga, George Nyangusu alisema baadhi ya walimu wamekata tamaa, hivyo hufundisha ili kutimiza wajibu bila kujali iwapo wanafunzi wanaelewa wanachofundishwa.

“Walimu wanalazimika kutumia muda mwingi kwa shughuli za kujiongezea kipato ikiwamo kufundisha masomo ya ziada ili kumudu gharama za maisha zinazopanda kila kukicha,” alisema Nyangusu.