Canada kuzisaidia nchi za Afrika katika ujasiriamali, jinsia

Balozi wa Canada hapa nchini,Ian Myles

Muktasari:

  • Akizungumza leo(Jumatatu),Balozi wa Canada hapa nchini,Ian Myles amesema kuwa nchi hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuimarisha misingi ya demokrasia pamoja na kutatua migogoro mbalimbali.
  • "Ni vizuri kuwa watulivu na kuheshimu haki za binadamu ili kuimarisha amani kwa maendeleo ya uchumi,"alisema Myles.

Dar es Salaam.Katika kuadhimisha miaka 150 ya Shirikisho la Canada, Serikali ya nchi hiyo imesema itaendelea kuimarisha uhusiano wake na nchi za Afrika katika kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ikiwamo ya ukatili wa kijinsia  elimu ya ujasiriamali.

Akizungumza leo(Jumatatu),Balozi wa Canada hapa nchini,Ian Myles amesema kuwa nchi hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuimarisha misingi ya demokrasia pamoja na kutatua migogoro mbalimbali.

"Ni vizuri kuwa watulivu na kuheshimu haki za binadamu ili kuimarisha amani kwa maendeleo ya uchumi,"alisema Myles.

Aidha,nchi hiyo pamoja na zile zinazozungumza lugha ya Kifaransa barani Afrika "Francophone" zimekuwa zikisaidiana katika kutoa mafunzo na elimu ya ujasiriamali ili kupunguza tatizo la ajira.