Chadema, ACT-Wazalendo waijibu CCM

Msemaji wa chama tawala, Christopher ole Sendeka .

Muktasari:

  • Chadema kwenye mkutano na waandishi wa habari iliijibu CCM ikisema chama hicho kinaugua ugonjwa wa ‘Lowassaphobia’ na kwamba waziri huyo mkuu wa zamani ni tishio na ataendelea kuwa tishio kwao.

Dar es Salaam. Chadema na ACT-Wazalendo hutofautiana kwa mengi, lakini jana waliungana kuitolea uvuvi CCM baada ya msemaji wa chama hicho tawala, Christopher ole Sendeka kuwazungumzia vibaya Edward Lowassa na Zitto Kabwe.

Chadema kwenye mkutano na waandishi wa habari iliijibu CCM ikisema chama hicho kinaugua ugonjwa wa ‘Lowassaphobia’ na kwamba waziri huyo mkuu wa zamani ni tishio na ataendelea kuwa tishio kwao.

Habari zinazohusiana

ACT-Wazalendo, ambayo pia ilifanya mkutano na waandishi wa habari ilisema tuhuma zilizotolewa na CCM kumuhusisha Zitto na sakata la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ni hoja nyepesi, na kwamba kama anahusika afikishwe mahakamani ili ukweli ubainike.