Friday, February 17, 2017

Chadema kuendeleza maazimio ya Ukuta

Makamu mwenyekiti wa chama wa Chadema, Profesa

Makamu mwenyekiti wa chama wa Chadema, Profesa Abdallah Safari 

By Kalunde Jamal, Mwananchi

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kuendeleza maazimio ya Ukuta kwa sababu waliyoyatabiri ndiyo yanayotokea sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema lengo la ukuta lilikuwa endelevu nz lenye lengo la kukemea udikteta nyemelezi.

Alisema yale yaliyokuwa yakipingwa ndiyo yanajitokeza sasa, hivyo ni wakati wa kuuamsha kwa nguvu moja.

-->