Chadema wabadili gia

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Muktasari:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza mikakati mitatu ya kupinga ukandamizaji wa haki na demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza mikakati mitatu ya kupinga ukandamizaji wa haki na demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali.

Moja ya mikakati ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini ni kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini nzima Septemba Mosi mwaka huu.

 “Kwa sababu wenzake hawamuelezi, sisi (Chadema) tunamueleza (Rais John Magufuli). Mtaona sisi hatutakuwa salama,  inawezekana tusiwe salama, lakini leo itakuwa zamu yetu na kesho zamu yenu na hatimaye nchi hii haitakuwa salama. Iweje sisi tusifanye mikutano ya hadhara yeye afanye,” alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam jana.

Zaidi soma ndani ya gazeti letu la Mwananchi