Chadema wahofia CCM kupendelewa

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu 

Muktasari:

Kutokana na hali hiyo, Chadema imedai uamuzi wa polisi kuruhusu mikutano ya ndani unaibeba CCM inayotarajia kuianza hivi karibuni.

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amedai kuwa ana taarifa CCM imepanga vikao vyake vya ndani ndiyo maana polisi imeondoa zuio hilo.

Kutokana na hali hiyo, Chadema imedai uamuzi wa polisi kuruhusu mikutano ya ndani unaibeba CCM inayotarajia kuianza hivi karibuni.

Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani juzi alitangaza kuruhusu mikutano ya ndani iliyoizuia tangu Agosti 24 baada ya kujiridhisha na hali ya usalama nchini.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka  amesema taarifa ya polisi haikutaja chama kimoja bali imeeleza vyama vyote vinaruhusiwa kufanya vikao au mikutano ya ndani.