Chadema walia na sheria, katiba

Muktasari:

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Vedastus Patrick alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ofisi mkoa eneo la Igoma wilayani Nyamagana.

Hali ya siasa nchini imekuwa tete huku sheria na katiba hazizingatiwi na viongozi walioko madarakani, imeelezwa.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Vedastus Patrick alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ofisi mkoa eneo la Igoma wilayani Nyamagana.

Patrick alisema, watu waliopo upinzani, kwa sasa wanapitia wakati mgumu wa kuwindwa mchana na usiku ili kunyamazishwa na wasiojulikana huku wakiwa katika harakati za kutafuta haki.

Alisema lengo la Chadema ni kumiliki dola kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020 ili kuboresha sekta ambazo zimeanza kuathirika kwenye hii Serikali.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza, Susane Maselle, ambaye alinunua kiwanja cha ujenzi wa ofisi hiyo, alisema ni jukumu la wajumbe na wafuasi wote wa Chadema kuhakikisha ujenzi huo unaanza ili kuboresha huduma za chama. (Jonathan Musa)