Chadema wamvua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya

Muktasari:

Saadat  ambaye alikuwa mwenyejkiti wa wilaya kwa kipindi kirefu, alisimamishwa wadhifa huo Juni mwaka huu.

Mbeya. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Kyela mkoani hapa kimemvua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kyela, Saadat Mwambungu kwa tuhuma za kufanya mambo kinyume na katiba.

Saadat  ambaye alikuwa mwenyejkiti wa wilaya kwa kipindi kirefu, alisimamishwa wadhifa huo Juni mwaka huu.

Katibu wa Chama wa wilaya hiyo, Mponjoli Mwaikimba alisema jana kwa njia ya simu kwamba kamati tendaji ya chama sasa imemvua uanachama na nyadhifa zingine zote.

Saadat Mwambungu alipoulizwa jana kwa simu kuhusu kuvuliwa uanachama alisema alisikia kupitia vyombo vya habari, lakini hadi jana alikuwa bado kupata barua rasmi.

 “Mimi kama Saadat sitambui uamuzi uliotolewa na kamati tendaji kwani imekiuka katiba ya chama,’’alisema.