Mbowe atinga kwenye jimbo la Lissu

Muktasari:

Viongozi wa Chadema waliopo kwenye kampeni z a udiwani wamesema wako tayari kugharamia matibabu ya Lissu hata kwa kuuza Figo.

Singida. Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza leo  Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema amesema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Amesema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" amesema Lema.

Amesema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.