Monday, July 17, 2017

Chadema yatangaza vita na CUF ya Lipumba

 

By Asna Kaniki, Mwananchi; mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Tundu Lissu amesema Ukawa wanatangaza vita na CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba kama walivyo vitani na CCM ya Rais John Magufuli.

Lissu ameyasema hayo leo (Jumatatu Julai 17) wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho.

Lissu amesema Profesa Lipumba amewasaliti kwa kuwa yeye ndiye aliyempitisha Lowassa (Edward) kuwa mgombea wa uraisi kwa tiketi ya Ukawa

"CUF ya Lipumba ilitusaliti kama Yuda Iskariot alivyomsaliti Yesu,"amesema Lissu.

Pia Lissu amelishauri jeshi la polisi kuacha kupambana na upinzani na badala yake wakapambane na wahalifu wanaofanya mauaji Kibiti.

-->