Cheyo, Mrema wapingwa kuitetea CCM

Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha  TLP,Augustine Mrema akiwa na John Cheyo (UDP) .

Muktasari:

  • Katika mkutano huo, Mrema alisema, “CCM msione mkipeta ni kwa sababu ya upendo na ukarimu wenu. Mwaka 2009 nilikuwa mgonjwa ni wewe Jakaya (Kikwete) ulinipeleka India na mke wangu kutibiwa.”
  • Kadhalika, Cheyo alisema ni vigumu kuiondoa CCM madarakani na kuwa siasa si ugomvi kama ambavyo baadhi ya vyama vya upinzani vimekuwa vikifanya.

Dar es Salaam. Wasomi na wanasiasa nchini wamekosoa kauli za viongozi wa vyama vya siasa, John Cheyo (UDP) na Augustine Mrema (TLP) walizozitoa katika Mkutano Mkuu wa CCM kinyume na malengo ya vyama vyao.

Katika mkutano huo, Mrema alisema, “CCM msione mkipeta ni kwa sababu ya upendo na ukarimu wenu. Mwaka 2009 nilikuwa mgonjwa ni wewe Jakaya (Kikwete) ulinipeleka India na mke wangu kutibiwa.”

Kadhalika, Cheyo alisema ni vigumu kuiondoa CCM madarakani na kuwa siasa si ugomvi kama ambavyo baadhi ya vyama vya upinzani vimekuwa vikifanya.

“Chama cha Mapinduzi ni kigumu kuking’oa. Huwezi kuing’oa CCM kwa kususia vikao vya Bunge. Siasa siyo ugomvi, siyo uadui,” alisema Cheyo alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo.

Zaidi soma gazeti la Mwananchi leo