China kuunga mkono harakati za kuhamia Dodoma.

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, alisema pia wataendeleza ujenzi wa jengo jingine la wizara hiyo jijini hapa ambalo litatumika kwa shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.

Dar es Salaam. Serikali ya China imeahidi kujenga jengo la Wizara ya Mambo ya Nje mjini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, alisema pia wataendeleza ujenzi wa jengo jingine la wizara hiyo jijini hapa ambalo litatumika kwa shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.

Waziri Yi alisema hayo jana baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambayo yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga.

Alisema Serikali ya China itajenga bandari za Bagamoyo na Zanzibar na itaiboresha Reli ya Tazara na Reli ya Kati.