China yaipiga tafu wizara ya habari na Sanaa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Muktasari:

Akipokea msaada huo leo (Jumatano), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Petro Lyatuu amesema msaada huo utachangia  katika kuinua  wasanii wa Tanzania.

Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya Sh20 milioni kutoka ubalozi wa China  kwa ajili ya kukuza idara ya sanaa.

Akipokea msaada huo leo (Jumatano), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Petro Lyatuu amesema msaada huo utachangia  katika kuinua  wasanii wa Tanzania.

"Kuna mikakati mingi imewekwa kuinua wasanii wetu ikiwemo mfuko maalum utakaowasaidia wale wenye kipato kidogo, sera itakayowalinda na hata hivi vifaa vitasaidia kurahisisha utoaji huduma kwao," amesema Lyatuu.