Friday, May 19, 2017

China yazuia ndege za Marekani

 

By Washington, Marekani

Washington, Marekani. Jeshi la Marekani limekiri kuwa ndege yake imezuiwa na ndege mbili za China kuendelea na safari ya uchunguzi ili kugundua mionzi katika anga la kimataifa lililoko mashariki mwa Bahari ya China.

Leo la Marekani kutuma ndege hiyo ilikuwa kupata ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia yaliyofanywa hivi karibuni na Korea Kaskazini.

China imekuwa ikipinga shughuli za Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake na kwamba husababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.

''Suala hilo linashughulikiwa na China kwa kutumia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi,” alisema msemaji wa jeshi la anga la Marekani Luteni kanali Lori Hodge.

“Uzuiaji huu haukufanyika kwa njia za kitaalamu kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili,” aliongeza.

Februari mwaka huu Marekani ilirusha ndege yake moja katika kile ilichoelezea kuwa ni doria yake ya kawaida kusini mwa bahari hiyo huku ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.

 

 

-->