VIDEO: Costech yasikitika barua waliyowaandikia Twaweza kusambaa mitandaoni

Thursday July 12 2018

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH), Dk Amos Nungu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kusikitishwa na kusambaa mitandaoni kwa  barua walioandikia taasisi ya utafiti ya Twaweza. Kulia ni Mwanasheria wa tume hiyo, Zainab Bakari na kushoto ni Mtafiti wa tume hiyo, Mashuhuri Mwinyihamis. Picha na Ericky Boniphace 

By Ibrahim Yamola, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imesikitishwa na kitendo cha barua yake kwenda Taasisi ya Utafiti ya Twaweza kusambaa mitandaoni.

Costech imesema hayo leo Julai 12, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dk Amos Nungu amesema baada ya kufuatilia, wamebaini barua hiyo  waliyowaandikia Twaweza ni ya kwao.

"Tunasikitika kuona mawasiliano halali ya kiofisi yanapelekwa mitandaoni, hata kabla ya kujibiwa rasmi," amesema Dk Nungu

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema barua hiyo si ya kwanza na wamekuwa wakiandika kwenda kwa wadau mara kadhaa.

Naye Mwanasheria wa Costech, Zainab Bakari ameshindwa kufafanua vifungu vya sheria walivyotumia akisema:

"Hatujaja hapa kuzungumzia barua ya Twaweza."

Soma Zaidi:

Utafiti Twaweza waibua mapya

Costech yailima barua Twaweza