DC Arumeru azuia malipo ya posho

Muktasari:

  • Halmashauri hizo ni Meru na Arusha DC  ambazo zinaongozwa na Chadema.

Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti amewapiga marufuku wakurugenzi wa halmashauri mbili ndani ya wilaya hiyo kuwalipa madiwani Sh40,000 za nauli bali walipwe nauli elekezi za Sumatra kwa lengo la kuokoa fedha za kuwahudumia wananchi.

Halmashauri hizo ni Meru na Arusha DC  ambazo zinaongozwa na Chadema.

Mgogoro wa posho pia umekwishajitokea katika Halmashauri wa Manispaa ya Arusha ambayo pia inaongozwa na chama hicho, jambo ambalo liliwagonganisha Mbunge wa arusha Mjini, Godbless Lema na  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo ambaye hivi karibuni alipandishwa cheo kuwa mkuu wa mkoa.