DC Bahi apiga marufuku maandamano ya Ukuta

Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema Taifa

Muktasari:

Ametoa amri hiyo kwenye Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo na kusisitiza kuwa hataki kusikia kitu kinachoitwa maandamano.

Bahi. Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Elizabeth amepiga marufuku maandamano ya vyama pinzani ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) yatakayofanyika Septemba badala yake wananchi wameagizwa kuitumia siku hiyo kufanya kazi.

Ametoa amri hiyo kwenye Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo na kusisitiza kuwa hataki kusikia kitu kinachoitwa maandamano.

 “Naagiza Septemba Mosi kila mmoja afanye kazi za kujiletea maendeleo, tuachane na vitu visivyokuwa na tija, hasa vijana wetu,” amesema Kitundu.

Hata hivyo, amri hiyo imepingwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Jelly Mambo akisema maandamano yao yapo palepale na hakuna kilichobadilika kwani wamekamilisha maandalizi yao na kuwataka watu kujitokeza.