DC Hapi aagiza Corner Bar ifungwe

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi

Muktasari:

Akiwa katika ziara ya kawaida leo (Jumamosi) mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama  kuifunga baa hiyo.

Dar es Salaam. Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika  baa maarufu ya Corner, sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.

Akiwa katika ziara ya kawaida leo (Jumamosi) mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama  kuifunga baa hiyo.

“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi vikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya...natoa agizo kesho.nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa  inakiuka maadili,”amesema Hapi.

Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.

“ Mkuu hii baa ni sugu, nimeahawahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia kesho itakuwa tayari,” amesema.