DC aanza utekelezaji agizo la JPM

Muktasari:

Alitoa agizo hilo kwa maofisa hao wakati akiwa katika ziara ya kukagua usafi wa mazingira katika kata hiyo.

Hata hivyo, muda uliokuwa umetolewa na Nkulu ulikwisha huku taka hizo zikiendelea kuwapo eneo hilo, jambo lilimlazimu kumuagiza mkuu wa polisi wa wilaya hiyo kuwakamata na maofisa hao na kuwaweka ndani.

Kahama. Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Fadhili Nkulu amewaweka mahabusu kwa saa tano maofisa wawili wa Halmashauri ya Mji Kahama baada ya kukaidi agizo lake la kufanya usafi eneo la Kata ya Nyasubi.

Nkulu aliagiza maofisa hao kuondoa mara moja taka laini zilizokuwa zimerundikwa  eneo la halmashauri hiyo, ambalo siyo sehemu maalumu ya kuwekea taka hizo lakini hawakutekeleza.