DC aliyeshurutisha wananchi kulipa michango afuta amri yake

Muktasari:

Mwambe ametakiwa kufuta amri hiyo kwa sababu  imeleta usumbufu kwa wakazi wa Manyoni, ambao wameona ni kama kurudishwa kodi ya kichwa.

Manyoni. Mkuu  wa Wilaya ya Manyoni, Geoffrey Mwambe amefuta amri ya kutaka wananchi kuchangia maendeleo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe.

Mwambe ametakiwa kufuta amri hiyo kwa sababu  imeleta usumbufu kwa wakazi wa Manyoni, ambao wameona ni kama kurudishwa kodi ya kichwa.

Septemba 6, Mwambe alitoa amri iliyoweka viwango vya uchangiaji kwa wananchi ikiwamo Sh15,000 kwa mtu; ng’ombe na punda Sh3,000; mbuzi na kondoo Sh2,000.